KUITWA KWENYE USAILI WA AJIRA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

KUITWA KWENYE USAILI WA AJIRA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

🔥 KUITWA KWENYE USAILI WA AJIRA – JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI 🔥

Kutoka: Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Tarehe: 12 Disemba, 2025

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anawatangazia rasmi vijana wote walioomba ajira kupitia mfumo wa ajira.zimamoto.go.tz kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 15 Disemba, 2025 hadi 20 Disemba, 2025.

Usaili wote utaanza saa 1:00 Asubuhi kila siku.


1. WAOMBAJI WENYE ELIMU YA KIDATO CHA NNE (FORM FOUR)

  • Tarehe ya Usaili: 15 Disemba, 2025
  • Kituo cha Usaili: Usaili utafanyika katika mikoa uliyochagua wakati wa kutuma maombi.

2. WAOMBAJI WENYE ELIMU YA SHAHADA NA TAALUMA MBALIMBALI

Usaili kwa waombaji wa Shahada na taaluma mbalimbali utafanyika katika Ukumbi wa Andengenye – Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Dodoma.

  • Tarehe 15 hadi 17 Disemba, 2025:
    • Walioomba kwa taaluma ya Michezo (Sportsmen) watafanyiwa usaili.
    • Wamegawanywa katika makundi matatu (03): Kundi A litafanya usaili tarehe 15 Disemba, Kundi B tarehe 16 Disemba, na Kundi C tarehe 17 Disemba.
    • Makundi haya yameoneshwa kwenye kiambata kilichopo kwenye tovuti.
  • Tarehe 18 Disemba, 2025:
    • Walioomba kwa taaluma ya Emergency Medical Technician na Nursing.
  • Tarehe 19 Disemba, 2025:
    • Walioomba kwa taaluma ya Uzamiaji (Diver).
  • Tarehe 20 Disemba, 2025:
    • Walioomba kwa taaluma zifuatazo: Fire Fighting and Rescue Profession, Avionics, Civil Engineer, Data Scientist, Motor Vehicle Mechanics, Quantity Surveyor, Marine Engineer, Oil and Gas Engineer, Office Management Secretary, ICT Technician, ICT Network Technician na Madereva.

MAAGIZO MUHIMU KWA WASAILIWA WOTE

  • Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye kituo cha usaili siku na tarehe aliyopangiwa.
  • Fika na vyeti vyote halisi (Originals) vilivyotumika kwenye maombi ya ajira, ikiwemo: Cheti cha Kidato cha Nne, Cheti cha Kidato cha Sita (kama kinahusika), Cheti cha Taaluma, Cheti cha Kuzaliwa, pamoja na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
  • Kwa walioomba nafasi ya Udereva, wanatakiwa kuja na Leseni Halisi ya Udereva Daraja E.
  • Gharama zote za usafiri, chakula, na malazi ni juu ya msailiwa kwa muda wote atakaokuwa kwenye usaili.
See also  Tangazo La Kuitwa Kwenye Usaili MDAs na LGAs December 2025

Orodha kamili ya vijana waliochaguliwa kufanya usaili pamoja na makundi yao inapatikana kupitia tovuti ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji:

🌐 www.zimamoto.go.tz

BOFYA HAPA KUPAKUA ORODHA KAMILI YA MAJINA

Imetolewa na;

Kamishna Jenerali

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Makao Makuu Dodoma

12 Disemba, 2025

BOFYA HAPA KUPAKUA ORODHA KAMILI YA MAJINA

Spread the love

About Author

Here to ease your search for new opportunities. I am a person with a passion of sharing useful opportunities to interested Job seekers in a timely and accurate manner, aiming to ease the Job Search experience.