
Website TBS
Tanzania Bureau of Standards (TBS) is Tanzania’s sole Standards body,
Tangazo la Nafasi za Kazi TBS: Fundi Mchundo – Local Fundi
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatangaza nafasi za kazi za ufundi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kukagulia magari yanayoingia nchini, katika ofisi zake zilizopo Ubungo. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) anawatangazia wananchi wote wenye uwezo, sifa, na uzoefu wa ujenzi kuomba kazi hizi.
SIFA ZA MWOMBAJI (FUNDI MKUU)
- Ajue kusoma na kutafsiri michoro ya ujenzi.
- Awe na uwezo wa kusimamia kazi za ujenzi.
- Awe na ujuzi na uzoefu wa aina mbalimbali za ufundi.
- Mwombaji anapaswa kuwa na mafundi wa fani mbalimbali na sifa zilizotajwa.
- Awe raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 18.
- Awe tayari kufanya kazi wikendi na siku za mapumziko pale itakapolazimu.
- Cheti cha ufundi ni sifa ya ziada kwa mwombaji.
MASHARTI YA MAOMBI
- Barua ya maombi iandikwe na fundi mkuu akizingatia masharti ya kabrasha la zabuni.
- Fundi anatakiwa kuonyesha muda wa kumaliza kazi.
- Maombi yaambatane na picha ndogo (passport size) mbili za rangi.
- Maombi yote yaambatane na njia za mawasiliano kama vile namba za simu, barua pepe, au anwani za makazi.
- Barua ya mdhamini anayeishi Wilaya ya Ubungo mwenye mali zisizohamishika ni sharti.
- Fundi Mkuu anatakiwa kujaza Jedwali la bei ya ufundi (Schedule of Labor) ambalo linajumuisha gharama zake pamoja na mafundi wengine na wasaidizi.
- Nyaraka za zabuni zinapatikana Ofisi ya Manunuzi katika Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Ubungo.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mkono kwa anwani ifuatayo:
MKURUGENZI MKUU,
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA – TBS,
S.L.P. 9524,
UBUNGO, DAR ES SALAAM.
Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya Fax, Telex, Telegraphic system na posta hayatapokelewa.
MWISHO WA KUPOTEA MAOMBI
Mwisho wa kupokea maombi ni Jumanne, tarehe 12 Agosti, 2025, saa 9:30 Jioni.
Ufunguzi wa maombi utafanyika saa 10:00 Jioni katika Ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Ubungo.
PAKUA TANGAZO HILI KATIKA MFUMO WA PDF HAPA
How to have more Energy in the Morning & Boost your Productivity