Tangazo La Nafasi Za Ajira Kutoka Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji November 2025

Full Time
  • Full Time
  • Dodoma

Website Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji

Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Kifungu cha 14(4) cha Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sura ya 427, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Utumishi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji za mwaka 2008; anatangaza nafasi za ajira ngazi ya Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa vijana wenye sifa zifuatazo: –

1. Elimu ya Kidato cha Nne

Sifa za mwombaji:

a) Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa
b) Awe na Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA)
c) Awe na afya njema kimwili na kiakili
d) Asiwe na kumbukumbu za uhalifu
e) Awe hajaoa au kuolewa
f) Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (Tattoos)
g) Awe hajawahi kutumia aina yoyote ya madawa ya kulevya
h) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya taaluma ya Zimamoto na Uokoaji
i) Awe hajawahi kuajiriwa serikalini
j) Awe mwenye urefu usiopungua futi 5.7 kwa mwanaume na futi 5.4 kwa mwanamke
k) Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa
l) Awe tayari kufanyakazi popote atakapopangiwa baada ya kumaliza mafunzo
m) Umri kuanzia miaka 18 hadi 25.


2. Elimu ya Kidato cha Nne au Sita

Madereva wa magari makubwa, Wauguzi ngazi ya Stashahada, taaluma za Zimamoto na Uokoaji, Matabibu ngazi ya Stashahada, Mafundi mchundo wa magari, wazinamiaji na waogeleaji, Wanamichezo, Brass band, Waandishi Waendesha Ofisi, TEHAMA ngazi ya Stashahada na mafundi umeme wa ndege ngazi ya Stashahada.

Sifa za mwombaji

a) Sifa zote zilizoainishwa kwenye Aya ya 1 (a hadi l)
b) Umri kuanzia miaka 18 hadi 28
c) Wazinamiaji na waogeleaji watafanyiwa uhakiki kwa vitendo
d) Madereva, awe na leseni daraja E (watakaoitwa kwenye Usaili watafanyiwa uhakiki kwa vitendo kuendesha magari makubwa)


3. Elimu ya Shahada

Wahandisi Bahari, TEHAMA, Wahandisi wa Ndege, Wakadiriaji Majenzi (QS), Sheria (walihitimu shule ya sheria kwa vitendo), Mafuta na gesi, Wahandisi ujenzi, Wahandisi mitambo na Wahandisi umeme.

Sifa za mwombaji

a) Sifa zote zilizoainishwa kwenye Aya ya 1 (a hadi l)
b) Umri kuanzia miaka 18 hadi 28


4. Namna ya kuomba

Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ajira wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unaopatikana kupitia kioka cha
https://ajira.zimamoto.go.tz mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 03 Desemba, 2025.

Mwombaji aambatishe kwenye mfumo nyaraka zifuatazo:

a) Barua ya maombi iliyoandikwa kwa mkono na mwombaji kwenda kwa,
Kamishna Jenerali,
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
1 Mtaa wa Zimamoto,
S.L.P 1509,
41102 DODOMA.

b) Fomu ya uthibitisho wa siha njema kutoka kwa mganga wa serikali



📝 Vigezo na Nyaraka Muhimu Zinazohitajika

Hizi ni nyaraka za ziada zinazohitajika, ambazo huenda zinaendeleza orodha iliyotangulia:

  • c) Nakala ya Kitambulisho cha NIDA au namba yake.

  • d) Namba ya mtihani wa Kidato cha Nne.

  • e) Namba ya mtihani wa Kidato cha Sita.

  • f) Namba ya vyeti vya taaluma kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali katika ngazi ya Astashahada, Stashahada, au Shahada.

  • g) Namba ya kumbukumbu ya barua ya Utambulisho kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa (Kupitia mfumo wa NaPA).


⚠️ Mambo ya Kuzingatia (Zingatia)

Tafadhali zingatia masharti na taratibu zifuatazo muhimu wakati wa kuwasilisha maombi yako:

  • Uthibitishaji wa Nyaraka: Nakala za vyeti vingine kama vipo (vilivyotajwa kwenye aya ya 4(d), (e), na (f) ya tangazo kamili) lazima viambatishwe vikiwa vimethibitishwa na Kamishna wa Viapo au Hakimu.

  • Njia ya Kuwasilisha: Barua zitakazowasilishwa kwa njia ya posta, mkono, au kwa barua pepe hazitapokelewa (hii inamaanisha ni lazima utumie mfumo mahususi wa maombi).

  • Taarifa za Mawasiliano: Waombaji wote waandike namba za simu kwenye barua zao za maombi.

  • Uaminifu: Mwombaji atakayewasilisha nyaraka za kughushi au taarifa za uwongo atachukuliwa hatua za kisheria.

  • Uchunguzi wa Afya: Mwombaji atapimwa tena afya ya mwili na akili akifika Chuoni.


✒️ Taarifa za Mtoaji

Hati hii imetolewa na:

  • Tarehe: 19 Novemba, 2025

  • Jina: John W. Masunga

  • Cheo: KAMISHNA JENERALI

  • Taasisi: JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI


To apply for this job please visit ajira.zimamoto.go.tz.

Spread the love