912 Exciting Career Opportunities At Public Service Recruitment Secretariat (PSRS), Dodoma January 2026

Full Time
  • Full Time
  • Dodoma

Website Public Service Recruitment Secretariat (PSRS)

Public Service Recruitment Secretariat (PSRS)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Ref. No. JA.9/259/01/C/16
14 Januari, 2026

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 912 kama ilivyoainishwa hapa chini:


1.0 MWALIMU DARAJA LA III C – HISABATI (MATHEMATICS)

Nafasi: 709

1.1 Majukumu ya Kazi

i. Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na mpango wa kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
ii. Kutengeneza na kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
iii. Kufundisha, kufanya tathmini na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya wanafunzi;
iv. Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi shuleni na darasani;
v. Kusimamia malezi ya wanafunzi kiakili, kimwili, kiroho na kutoa ushauri nasaha;
vi. Kutoa ushauri wa kitaaluma kuhusu maendeleo ya elimu;
vii. Kusimamia na kutunza vifaa na mali za shule;
viii. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Shule.

1.2 Sifa za Mwombaji

  • Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la Hisabati
    AU
  • Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la Hisabati pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (PGDE) kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.

1.3 Ngazi ya Mshahara

TGTS – D


2.0 MWALIMU DARAJA LA III C – FIZIKIA (PHYSICS)

Nafasi: 201

2.1 Majukumu ya Kazi

(Majukumu ni sawa na yaliyoainishwa kwa Mwalimu wa Hisabati)

2.2 Sifa za Mwombaji

  • Shahada ya Elimu au Shahada ya Ualimu yenye somo la Fizikia
    AU
  • Shahada isiyo ya Elimu yenye somo la Fizikia pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (PGDE) kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.

2.3 Ngazi ya Mshahara

TGTS – D


3.0 MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (CHILD CARE ASSISTANT)

Nafasi: 2

3.1 Majukumu ya Kazi

i. Kushiriki kutekeleza mpango jumuishi wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (ECD);
ii. Kuandaa na kutekeleza ratiba ya shughuli za kila siku;
iii. Kubainisha na kutumia mazingira salama ya kujifunzia watoto;
iv. Kutoa rufaa kwa masuala ya watoto yaliyo nje ya uwezo wake;
v. Kutambua watoto wenye mahitaji maalumu na kutoa huduma stahiki;
vi. Kushiriki katika uhamasishaji wa jamii;
vii. Kutoa ushauri kwa wazazi/walezi;
viii. Kuandaa taarifa za utekelezaji wa shughuli;
ix. Kushiriki kwenye mchakato wa mashauri ya watoto (case management);
x. Kuandaa taarifa za uanzishaji wa vituo vya malezi;
xi. Kufanya kazi nyingine atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi.

3.2 Sifa za Mwombaji

  • Wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada ya Elimu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, Ustawi wa Jamii au Saikolojia kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.

3.3 Ngazi ya Mshahara

TGS – B


MASHARTI YA JUMLA

  1. Waombaji wawe raia wa Tanzania na wasizidi miaka 45.
    • Nafasi zisizo za shahada (taasisi za kijeshi): ≤ miaka 25
    • Nafasi za shahada: ≤ miaka 30
  2. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na waainishe ulemavu wao kwenye mfumo.
  3. Cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili kiambatishwe.
  4. Waajiriwa wa Utumishi wa Umma wasitume maombi.
  5. Maombi yaambatane na vyeti halisi vilivyothibitishwa.
  6. Testimonial, provisional results na result slips hazitakubaliwa.
  7. Waombaji waliosoma nje wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU/NECTA/NACTVET.
  8. Waliofukuzwa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali.
  9. Kugushi taarifa ni kosa la kisheria.
  10. Mwisho wa kutuma maombi: 28 Januari, 2026.
  11. Barua ya maombi ielekezwe kwa:

KATIBU
Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
S.L.P. 2320,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
Dodoma.

  1. Maombi yatumwe kupitia https://portal.ajira.go.tz
  2. Maombi nje ya utaratibu hayatazingatiwa.

Imetolewa na:
KATIBU
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma


To apply for this job please visit portal.ajira.go.tz.

Spread the love