JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Tarehe: 17 Novemba 2025
Mahali: Dodoma

Tume ya Utumishi wa Mahakama, iliyoanzishwa kwa mujibu wa Aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, inawatangazia Watanzania wenye sifa stahiki kuomba ajira katika kada mbalimbali za Mahakama ya Tanzania. Waombaji wanapaswa kuwa tayari kufanya kazi katika Mikoa na Wilaya mbalimbali nchini.


1.0 HAKIMU MKAZI II – TJS II

1.1 Sifa za Kuajiriwa

  • Cheti cha Kidato cha Nne/Sita
  • Shahada ya Sheria (LL.B) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali
  • Stashahada ya Uzamili ya Mafunzo ya Sheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania)
  • Cheti cha mafunzo ya kompyuta ni kipaumbele

1.2 Majukumu

  1. Kuandaa mpango wa mashauri ya awali (Jinai na Madai)
  2. Kusikiliza mashauri ya awali ya Jinai, Madai, Ndoa na Mirathi
  3. Kutoa hukumu za mashauri aliyosikiliza
  4. Kutoa amri mbalimbali za kimahakama
  5. Kusuluhisha mashauri
  6. Kusikiliza rufani kutoka Mabaraza ya Kata
  7. Kufanya utafiti wa kisheria na kutoa ushauri
  8. Majukumu mengine atakayopangiwa

2.0 AFISA UTUMISHI II – TGS E

2.1 Sifa za Kuajiriwa

Shahada katika:

  • Human Resources Management
  • Human Resources Planning
  • HR Planning & Management
  • Labour Relations & Public Management
  • Industrial Relations
  • Business Administration / Commerce (HRM)

2.2 Majukumu

  • Kutunza kumbukumbu za watumishi
  • Kutafsiri na kushughulikia miundo ya utumishi
  • Kupanga na kukadiria mahitaji ya mafunzo ya watumishi
  • Kukusanya na kuchambua takwimu za rasilimali watu
  • Kushughulikia masuala ya kila siku ya watumishi

3.0 MHASIBU II – TGS E

3.1 Sifa za Kuajiriwa

  • Shahada ya Biashara/Sanaa iliyo na Uhasibu
  • Au Stashahada ya Juu ya Uhasibu
  • Cheti cha Taaluma ya Uhasibu CPA (T) – NBAA

3.2 Majukumu

  • Kuandaa taarifa za mapato na matumizi
  • Kuandaa taarifa za maduhuli
  • Kupokea na kuwasilisha maduhuli Benki
  • Usuluhisho wa hesabu za Benki na fedha
  • Kuhakiki hati za malipo

4.0 AFISA UGAVI MSAIDIZI I – TGS C

4.1 Sifa za Kuajiriwa

  • Stashahada ya Ununuzi/Ugavi au Biashara (Ununuzi & Ugavi)
  • Usajili na PSPTB kama Procurement and Supplies Full Technician
  • Ujuzi wa kompyuta

4.2 Majukumu

  • Kutunza na kupanga vifaa ghalani
  • Kupokea vifaa kutoka kwa wazabuni
  • Kutunza vifaa vilivyotumika
  • Kufungua Bin Card na Ledger
  • Kutoa vifaa kwa watumiaji
  • Kazi nyingine za fani husika

5.0 AFISA UNUNUZI II – TGS D

5.1 Sifa za Kuajiriwa

  • Shahada/Stashahada ya Juu ya Ununuzi/Ugavi
  • Au Professional Level III (PSPTB)
  • Usajili: Graduate Procurement & Supplies Professional

5.2 Majukumu

  • Kuandaa matangazo ya zabuni
  • Kusambaza nyaraka za zabuni
  • Kuwasiliana na idara kuhusu mahitaji
  • Kukusanya taarifa za bei (market intelligence)
  • Kuhakiki hati za madai
  • Kazi nyingine za fani husika

6.0 AFISA UGAVI II – TGS D

6.1 Sifa za Kuajiriwa

(Vigezo sawa na Nafasi ya 5.0)

6.2 Majukumu

  • Kutayarisha makisio ya vifaa
  • Kuandaa utaratibu wa upokeaji wa vifaa
  • Kukusanya takwimu za vifaa
  • Kusimamia upokeaji, utunzaji na usambazaji
  • Kubuni mifumo ya uwekaji vifaa ghalani

7.0 KOMPYUTA OPARETA II – TGS C

7.1 Sifa za Kuajiriwa

  • Stashahada ya Kompyuta kutoka chuo kinachotambuliwa
  • Uzoefu wa miaka 3

7.2 Majukumu

  • Kufanya kazi za mifumo ya kompyuta yenye ugumu wa wastani
  • Kutunza mpango wa kazi katika chumba cha kompyuta
  • Kutunza vitabu vya matumizi
  • Kuhifadhi data
  • Kuchapa taarifa za mwisho
  • Kuratibu maandalizi ya vikao

8.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – TGS C

8.1 Sifa za Kuajiriwa

  • Kidato cha Nne/Sita
  • Diploma ya Uhazili / NTA Level 6
  • Uandishi wa maneno 100 kwa dakika (Kiswahili & Kiingereza)
  • Ujuzi wa Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email, Publisher

8.2 Majukumu

  • Kuchapa barua na nyaraka
  • Kupokea wageni
  • Kutunza kumbukumbu, miadi na taarifa
  • Kutafuta na kusambaza majalada
  • Kutayarisha dondoo na maandalizi ya vikao

9.0 MPISHI – TGS C

9.1 Sifa za Kuajiriwa

  • Kidato cha Nne
  • Cheti cha Food Production (angalau mwaka mmoja)
  • Uzoefu wa miaka 3

9.2 Majukumu

  • Kusafisha jiko
  • Kupika chakula cha kawaida

10.0 DEREVA II – TGS B

10.1 Sifa za Kuajiriwa

  • Kidato cha Nne
  • Leseni Daraja la E au C1
  • Uzoefu wa uendeshaji angalau mwaka 1 bila ajali
  • Mafunzo ya Basic Driving Course (VETA au chuo kinachotambuliwa)
  • Cheti cha Ufundi Daraja la II ni kipaumbele

10.2 Majukumu

  • Kukagua gari kabla/baada ya safari
  • Kuwapeleka watumishi safari za kikazi
  • Matengenezo madogo madogo
  • Kusambaza nyaraka
  • Kutunza taarifa za safari
  • Kufanya usafi wa gari

11.0 MLINZI – TGOS A

11.1 Sifa za Kuajiriwa

  • Kidato cha Nne (Kiswahili & Kiingereza ufaulu)
  • Cheti cha mafunzo kutoka:
    • JKT
    • Polisi
    • Zimamoto
    • Mgambo
    • Au taasisi inayotambuliwa na Serikali

11.2 Majukumu

  • Kudhibiti mali zinazoingia/kutoka langoni
  • Kulinda majengo na mali za ofisi
  • Kuangalia milango/madirisha mwisho wa kazi
  • Kudhibiti uingiaji wa wageni
  • Kupambana na majanga na kutoa taarifa
  • Kutoa ushauri wa kuboresha ulinzi

12.0 MSAIDIZI WA OFISI – TGOS A

12.1 Sifa za Kuajiriwa

  • Kidato cha Nne
  • Mafunzo mafupi ya Office Attendant / Office Management n.k.

12.2 Majukumu

  • Kusafisha ofisi na mazingira
  • Kuchukua/kurejesha majalada
  • Kusambaza barua
  • Kutayarisha chai
  • Kupeleka/kuchukua posta
  • Kudurufu nyaraka
  • Kufungua na kufunga ofisi
  • Kutunza vifaa vya ofisi

13.0 MAELEZO MUHIMU KWA WAOMBAJI

  1. Awe Mtanzania
  2. Maombi yote yawasilishwe kielektroniki kupitia: www.jsc.go.tz
  3. Wakati wa kujaza fomu hakikisha unapakia:
    • Barua ya maombi iliyosainiwa
    • Vyeti vya elimu, mafunzo na matokeo
    • Cheti cha kuzaliwa
    • Picha ya rangi (passport size)
    • Kitambulisho cha NIDA
    • Nyaraka nyingine kama fomu itakavyoelekeza
  4. Nafasi hizi ni kwa ajira mpya tu – watumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
  5. Umri: miaka 18–45
  6. Waombaji waliowahi kufukuzwa kazi hawataruhusiwa
  7. Waliosoma nje ya nchi lazima wahakikishe vyeti (NACTE/TCU)
  8. Taarifa za uongo zita lead hadi hatua za kisheria
  9. Waombaji wenye ulemavu watapewa kipaumbele
  10. Mwisho wa kutuma maombi: 29 Novemba 2025
  11. Mawasiliano kwa msaada:

Imetolewa na:

Lydia Churi
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Tume ya Utumishi wa Mahakama


CLICK HERE TO APPLY: