
Website NAOT
Kabla ya uhuru wa Tanganyika Ofisi ilifahamika kama Idara ya Ukaguzi ndani ya Tanganyika na Kiongozi wa Ofisi hiyo alitambulika kama Mkurugenzi wa Ukaguzi. Mkurugenzi huyo aliteuliwa na Katibu wa Jimbo au Gavana Mkuu kwa maelekezo ya Katibu wa Jimbo kwa niaba ya Mfalme au Malkia wa Uingereza.
Fursa za Ajira NAOT: Nafasi 73 za Ajira – Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza jumla ya nafasi 73 za kazi. Tangazo hili lilitolewa tarehe 08 Agosti, 2025.
Nafasi Zinazotangazwa:
- Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Hesabu) – Nafasi 55
- Majukumu: Kushiriki katika kuainisha maeneo ya ukaguzi, kuandaa mpango wa ukaguzi, kukagua nyaraka za matumizi na mapato ya Serikali, na kuandaa hoja na barua za ukaguzi.
- Sifa za Waombaji: Shahada ya kwanza ya Biashara/Sanaa yenye mwelekeo wa Uhasibu au Stashahada ya Juu ya Uhasibu (Advanced Diploma in Accounting). Shahada ya kwanza/Stashahada ya Sayansi ya Menejimenti ya Kodi (Bachelor of Science in Tax Management) kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali pia inakubalika.
- BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI YA AJIRA ZA – MKAGUZI DARAJA LA II (UKAGUZI WA HESABU) – 55 POST
- Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Usalama wa Mifumo ya TEHAMA) – Nafasi 5
- Majukumu: Kushiriki katika kuainisha maeneo ya mifumo ya habari yanayoweza kufanyiwa ukaguzi, kuandaa mpango kazi wa ukaguzi, na kufanya ukaguzi kwa vitendo. Pia wanashiriki katika kuchanganua taarifa na kuandaa rasimu ya taarifa ya ukaguzi.
- Sifa za Waombaji: Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu katika Usalama wa Mtandao (Bachelor of Cyber Security), Usalama wa Mifumo ya TEHAMA (Bachelor of ICT Security) au Usalama wa Mtandao wa Kompyuta (Bachelor of Computer Network Security). Waombaji pia wanapaswa kuwa na cheti cha Certified Ethical Hacker (CEH) au Cisco Certified Network Associate in Security (CCNA).
- BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI YA AJIRA ZA MKAGUZI DARAJA LA II ( UKAGUZI YA USALAMA WA MIFUMO YA TEHAMA) – 5 POST
- Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Kiuchunguzi Fani ya Utengenezaji wa Programu za TEHAMA) – Nafasi 1
- Majukumu: Kushiriki katika kuainisha maeneo ya ukaguzi wa kiuchunguzi, kuandaa mipango kazi, na kukusanya taarifa kwa ajili ya ukaguzi. Majukumu mengine ni pamoja na kusaidia katika kuandaa ripoti za ukaguzi na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo ya kaguzi zilizokwishafanyika.
- Sifa za Waombaji: Shahada ya kwanza /Stashahada ya Juu ya TEHAMA katika utengenezaji wa programu za mifumo ya TEHAMA kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali. Pia wanahitajika kuwa na uelewa na ujuzi wa vitendo katika Java EE, C#, C++, na Python, pamoja na uwezo wa kufanya kazi za Mifumo ya Uhifadhi Data zenye Uhusiano (Relational DataBase Management Systems).
- BOFYA HAPAT KUTUMA MAOMBI YA AJIRA YA MKAGUZI DARAJA LA II (UKAGUZI WA KIUCHUNGUZI FANI YA UTENGENEZAJI WA PROGRAMU ZA TEHEMA) – 1 POST
- Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi-Fani ya Usanifu wa Majengo) – Nafasi 1
- Sifa za Waombaji: Shahada ya kwanza /Stashahada ya Juu ya Usanifu wa Majengo (Bachelor of Architecture) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali na waliosajiliwa na Bodi za Usajili ya fani husika.
- BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI YA AJIRA YA MKAGUZI DARAJA LA II (UKAGUZI WA UFANISI- FANI YA USANIFU WA MAJENGO (ARCHITECTURE) – 1 POST
- Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi-Fani ya Uhandisi Mitambo) – Nafasi 1
- Sifa za Waombaji: Shahada ya kwanza /Stashahada ya Juu ya Uhandisi Mitambo (Bachelor of Mechanical Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
- BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI YA AJIRA YA MKAGUZI DARAJA LA II (UKAGUZI WA UFANISI- FANI YA UHANDISI WA MITAMBO (MECHANICAL ENGINEER) – 1 POST
- Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi-Fani ya Uchumi) – Nafasi 3
- Sifa za Waombaji: Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu katika mojawapo ya fani za Sayansi ya Uchumi, Sayansi ya Takwimu, au Sayansi ya Uchumi Kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI YA AJIRA YA MKAGUZI DARAJA LA II (UKAGUZI WA UFANISI- FANI YA UCHUMI (ECONOMIST) – 3 POST
- Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi – Mhandisi wa Ujenzi) – Nafasi 3
- Sifa za Waombaji: Shahada ya kwanza/Stashahada ya Juu ya Sayansi katika fani ya Uhandisi wa Ujenzi (Bachelor of Science in Civil Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
- MKAGUZI DARAJA LA II (UKAGUZI WA UFANISI – MHANDISI WA UJENZI (CIVIL ENGINEER) – 3 POST
- Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi – Fani ya Uhandisi wa Migodi) – Nafasi 1
- Sifa za Waombaji: Shahada ya kwanza/Stashahada katika fani ya Sayansi ya Uhandisi wa Madini (Bachelor of Science in Mining Engineering) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
- BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI YA AJIRA YA MKAGUZI DARAJA LA II (UKAGUZI WA UFANISI – FANI YA UHANDISI WA MIGODI(MINING ENGINEERING ) – 1 POST
- Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi – Fani ya Mipango Miji) – Nafasi 1
- Sifa za Waombaji: Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu katika fani ya Sayansi ya Upangaji Miji na Maeneo ya Ardhi ((Urban and Regional Planning) kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
- BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI YA AJIRA YA MKAGUZI DARAJA LA II (UKAGUZI WA UFANISI – FANI YA MIPANGO MIJI (TOWN PLANNER) – 1 POST
- Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi- Fani ya Uhandisi wa Umeme) – Nafasi 1
- Sifa za Waombaji: Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu katika fani ya Sayansi ya Uhandisi wa Umeme (Bachelor of Science in Electrical Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
- BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI YA AJIRA YA MKAGUZI DARAJA LA II (UKAGUZI WA UFANISI- FANI YA UHANDISI WA UMEME (ELECTRICAL ENGINEER) – 1 POST
- Mkaguzi Daraja la II (Ukaguzi wa Ufanisi- Fani ya Uhandisi wa Mawasiliano) – Nafasi 1
- Sifa za Waombaji: Shahada ya Kwanza au Stashahada ya Juu katika fani mojawapo ya Sayansi ya Uhandisi wa Mawasiliano (Telecommunication Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
- BOFYA HAPA KUTUMA MAOMBI YA AJIRA YA MKAGUZI DARAJA LA II (UKAGUZI WA UFANISI- FANI YA UHANDISI WA MAWASALIANO (TELECOMMUNICATION ENGINEER) – 1 POST
Masharti ya Jumla:
- Waombaji wote lazima wawe Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45, isipokuwa kwa wale ambao tayari wako kazini Serikalini.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba na wanapaswa kuainisha ulemavu walionao kwenye mfumo wa maombi.
- “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results” na hati za matokeo za kidato cha nne na sita (Form IV and Form VI Results Slips) hazitakubaliwa.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika kama TCU, NECTA, na NACTE.
- Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 21 Agosti, 2025.
- Maombi yote yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kwenye anwani ifuatayo: http://portal.ajira.go.tz/. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu huu hayatafikiriwa.
Kwa maelezo zaidi, soma tangazo kamili lililotolewa na Katibu, Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma.
Madeni App: Mfumo Bora wa Kudai Madeni Uliotamadal na Kujitegemea (Automatiki)
To apply for this job please visit portal.ajira.go.tz.