Madereva Wa Malori (Transit Drivers) at Usangu Logistics, Dar es Salaam January 2026

Full Time

Website Usangu Logistics

Possibility in every direction

Madereva Wa Malori (Transit Drivers) at Usangu Logistics

USANGU LOGISTICS (T) LTD

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI KWA MADEREVA WA MALORI (TRANSIT DRIVERS)

Uongozi wa USANGU LOGISTICS (T) LTD, unapenda kuwatangazia nafasi za kazi kwa Madereva wa Malori (Transit Drivers) wenye uzoefu wa kazi ili kujiunga na kampuni yetu.

Sifa za Muombaji:

  • Leseni halali ya Udereva daraja husika (E)

  • Cheti cha Udereva wa Malori kutoka Veta / NIT

  • Uelewa wa Sheria za Barabarani na taratibu za usalama barabarani

  • Umri kuanzia Miaka 25 hadi Miaka 45

  • Muombaji awe tayari kufanya kazi Ndani na Nje ya Tanzania.


NAKALA ZA KUAMBATANISHA NA MAOMBI YAKO:

NA MAELEZO YA NAKALA AMBATANISHI NA MAELEZO YA NAKALA AMBATANISHI
1 Barua ya maombi ya kazi iliyoandikwa kwa mkono na kuombewa 11 Namba ya simu ya mtandao wa Yas
2 Wasifu (CV) 12 Akaunti ya benki ya CRDB
3 Nakala za vyeti vinavyoonyesha elimu/uzoefu katika kazi husika 13 Barua za serikali za mtaa zinazotambulisha makazi ya wadhamini wa nje wawili (2) kutoka serikali ya mtaa
4 Nakala ya kitambulisho cha NIDA 14 Barua zilizoandikwa kwa mkono kutoka kwa wadhamini wa nje pamoja na picha zao
5 Nakala ya tin namba 15 Kopi ya kitambulisho cha NIDA cha mdhamini
6 Uthibitisho wa leseni ya Udereva 16 Barua za wadhamini wa ndani wawili (2) pamoja na picha za pamoja
7 Cheti cha alama za vidole inayotolewa na polisi (Police Clearance Report / Fingerprint) 17 Hati za udhamini wa ndani na nje (Affidavit of Guarantors)
8 Kopi ya kitambulisho cha NSSF 18 Picha tatu ndogo (Passport Size)
9 Barua ya serikali ya mtaa kuthibitisha makazi 19 Picha kubwa ya rangi moja (Coloured Current Full-Size Photographs)
10 Barua ya utambulisho kutoka kwa mwajiri wa zamani (Certificate of Service) 20 Hati ya Kusafiria ya Kitabu (Passport Book)

JINSI YA KUTUMA MAOMBI:

Wenye sifa tajwa hapo juu wawasilishe maombi yao ya kazi ofisi za USANGU LOGISTICS zilizopo; Tabata, Dar es Salaam kabla ya Tarehe: 15/02/2026.

Kwa Mawasiliano zaidi piga simu namba:

  • +255 755 011 492

  • +255 717 440 449


To apply for this job please visit .

Spread the love