Tangazo La Nafasi Za Internship (Paid Internship) Hafford Hospital August 2025.

Internship

Website Hafford Hospital

Hafford Hospital

Tangazo La Nafasi Za Internship (Paid Internship) Hafford Hospital August 2025.

HAFFORD HOSPITAL

Chang’ombe Maduka Mawili – Temeke, Dar es salaam – Tanzania (EA)

P.O.BOX 46246, DAR ES SALAAM. E-mail: haffordhealth@yahoo.com

TANGAZO LA NAFASI ZA INTERNSHIP (PAID INTERNSHIP)

Hospitali ya Hafford iliyopo Chang’ombe Maduka Mawili – Temeke, Dar es salaam Tanzania (EA) inatangaza nafasi za Internship kwa wahitimu wa kada zifuatazo:-

  1. AFISA MUUGUZI MSAIDIZI – NAFASI 4

    Sifa za Mwombaji

  2. Awe Mhitimu wa Stashahada/Diploma ya Uuguzi (Registered Nurse) kutoka chuo kinachotambuliwa na NACTE/TCU.
  3. Awe amesajiliwa na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) na kuwa na leseni halali ya kufanya kazi.
  4. Awe na uelewa wa huduma za msingi za uuguzi ikiwa ni pamoja na huduma kwa wagonjwa, utoaji wa dawa, na elimu ya afya.
  5. Uwezo wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wengine, kufuata maelekezo, na kuzingatia maadili ya kazi ya uuguzi.

    Vigezo vya Uchaguzi

    Kiwango cha ufaulu katika taaluma husika.

    Uzoefu wa kujitolea au attachment katika hospitali/kliniki (ikiwa upo).

    Nidhamu, mawasiliano mazuri, na uwezo wa kujifunza kwa haraka.

  6. MHUDUMU WA AFYA – NAFASI 03

    Sifa za Mwombaji

  • Awe mhitimu wa mafunzo ya uhudumu wa Afya (Medical Attendant/Nurse Attendant) kutoka chuo kinachotambuliwa na NACTE au VETA.
  • Awe na uelewa wa kazi za usaidizi katika huduma za afya, ikiwemo maandalizi ya wagonjwa, usafi wa mazingira ya kazi.
  • Awe na ari ya kujifunza, nidhamu, na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yenye presha.

Vigezo vya Uchaguzi

  • Kiwango cha ufaulu katika taaluma husika.
  • Mawasiliano mazuri na tabia njema kwa wagonjwa na wafanyakazi wenzake.
  • Utayari wa kufanya kazi katika muda unaopangwa na kufuata taratibu za afya na usalama kazini.
  1. MFAMASIA MSAIDIZI (PHARMACETICAL ASSISTANT) – NAFASI 01

    Sifa za Mwombaji

  2. Awe amehitimu ngazi ya Cheti (Certificate) katika taaluma ya Famasi (Pharmaceutical Sciences/Technology) kutoka chuo kinachotambulika na NACTE.
  3. Awe amesajiliwa na Baraza la Wafamasia Tanzania na mwenye leseni halali ya kufanya kazi.
  4. Awe na uelewa wa taratibu za hifadhi, utoaji na udhibiti wa dawa.
  5. Uwezo wa kuwasiliana vizuri na wagonjwa na watoa huduma wengine wa afya.

    Vigezo vya kuzingatia

  6. Uadilifu na maadili ya juu ya kazi.
  7. Uwezo wa kufanya kazi kwa timu na chini ya usimamizi mdogo.
  8. Utayari wa kujifunza na kufanya kazi katika mazingira yenye changamoto.
  9. Uwezo wa kutumia mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa dawa (mfano ELMIS au eHMS) utapewa kipaumbele.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE

  1. Awe raia wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18
  2. Awe na cheti halali cha kuzaliwa na nakala ya kitambulisho cha taifa (NIDA).
  3. Awe na vyeti halali vya kitaaluma kutoka vyuo vinavyotambulika na mamlaka husika (NACTE au NECTA kulingana na taaluma).
  4. Awe amesajiliwa na baraza au mamlaka husika ya taaluma (mfano: TNMC kwa Registered Nurse, Pharmacy Council kwa Msaidizi wa Famasia).
  5. Awe na maadili mazuri, nidhamu ya kazi na awe hana rekodi ya makosa ya jinai.
  6. Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wengine (teamwork) na chini ya usimamizi mdogo.
  7. Aheshimu na kutii maagizo ya viongozi na kufuata kanuni na taratibu za Taasisi/Hospitali
  8. Awe na uwezo wa kuwasiliana vizuri kwa Kiswahili na Kiingereza.
  9. Awe tayari kuanza kazi mara moja au ndani ya muda mfupi baada ya kupita kwenye usaili.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI

  • Kwa wahitimu wenye sifa na vigezo tajwa hapo juu watume nakala zifuatazo kupitia Whatsapp Namba 0712474448:
    1. Barua ya Maombi
    2. Nakala ya vyeti vya kitaaluma
    3. Leseni (kwa Registered Nurse)
    4. Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
    5. Nakala ya cheti cha usajili (Pharmacy Council)
    6. Wasifu Binafsi /CV
  • NB: Nakala zote ziwe kwenye pdf moja

Anuani ya barua iwe:-

HAFFORD HOSPITAL

AFISA RASILIMALI WATU,

P.O. BOX 46246

DAR ES SALAAM

S. L. P 46246,

DAR ES SALAAM.

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: 15 AUGUST 2025

See: To include a Photo or not to include a Photo on a CV ?

See also: CV Writing Services

Discover Reliable Cleaning & Home Services with Davis Enterprises!

To apply for this job please visit wa.link.

Spread the love