
Website Ideon Limited
Ideon Limited
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.
IDEON LIMITED inatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo kwa ajili ya kituo chake kilichopo Mbezi Beach, Dar es Salaam:
1. Msimamizi wa Wafanya Usafi (1 Nafasi)
Majukumu Makuu:
- Kusimamia kazi za kila siku za wafanya usafi.
- Kugawa majukumu na kuhakikisha maeneo yote yanasafishwa ipasavyo.
- Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha viwango vya usafi vinafuatwa.
- Kuwalindisha na kuwaongoza wafanya usafi kuhusu kanuni za usalama na afya.
- Kuandaa taarifa fupi za kazi na maduhurio ya wafanyakazi.
Sifa na Uzoefu:
- Awe na angalau Cheti au Diploma katika Utawala wa Biashara, Usimamizi wa Hoteli, au fani nyingine inayohusiana.
- Uzoefu wa angalau mwaka 1-2 katika usimamizi au kazi za usafi.
- Uwezo mzuri wa kuongoza na kuwasiliana.
- Awe mwaminifu, mchapakazi na mwenye uwezo wa kufanya kazi bila kusimamiwa wa karibu.
Masharti ya Kazi:
- Eneo la kazi: Dar es Salaam – Mbezi Beach
- Mshahara: 180,000/= Tsh kwa mwezi (NET)
2. Wafanya Usafi (4 Nafasi)
Majukumu Makuu:
- Kusafisha na kutunza usafi wa maeneo yaliyopangwa kila siku.
- Kufanya kazi kwa kufuata ratiba na maagizo ya Msimamizi.
- Kutunza vifaa na kuhakikisha vinatumika kwa uangalifu.
- Kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni za usalama na afya.
Sifa na Uzoefu:
- Awe na angalau elimu ya msingi/sekondari.
- Awe na bidii, uaminifu na uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano.
- Uzoefu wa kazi za usafi utapewa kipaumbele.
Masharti ya Kazi:
- Eneo la kazi: Dar es Salaam – Mbezi Beach
- Mshahara: 150,000/= Tsh kwa mwezi (NET)
Namna ya Kutuma Maombi:
- Wasilisha CV yako kupitia barua pepe: info@ideon.co.tz
To apply for this job email your details to info@ideon.co.tz