KUITWA KWENYE MAFUNZO YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI – JANUARI 2026

KUITWA KWENYE MAFUNZO YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI - JANUARI 2026

KUITWA KWENYE MAFUNZO YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatangaza majina ya Vijana waliochaguliwa kuhudhuria mafunzo ya Uaskari ngazi ya Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Wahusika wanatakiwa kufika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chogo Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga kuanzia tarehe 19 hadi 21 Januari, 2026 bila kukosa; kwa ambaye hatafika chuoni kwa tarehe zilizotajwa hatapokewa na nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine.

Kufika chuoni teremka kituo cha Kabuku Wilaya ya Handeni kilichopo kilometa 12 kutoka chuoni. Chuo kimeandaa utaratibu maalumu wa kuwapokea kwa tarehe zilizotajwa, kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku.

Mhusika atajigharamia nauli ya kwenda, chakula na malazi kwa siku zote ambazo atakuwa hajapokewa Chuoni.

Mhusika aje na vyeti halisi vya masomo, taaluma au ujuzi alioombea, cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha NIDA au namba, barua ya utambulisho (NaPA), barua halisi aliyoombea kazi na leseni hai kwa walioomba nafasi ya udereva. Vyeti vyote viwe na nakala tatu kwa kila cheti. Aidha, vyeti hivyo vitakaguliwa na atakayebainika kuwa na cheti/vyeti vyenye kasoro atarudishwa.

Mhusika atakapofika chuoni awe tayari kupimwa tena afya ya mwili na akili, ambaye atabainika kuwa na tatizo la kiafya hataruhusiwa kuendelea na mafunzo na atarudishwa kwa gharama zake.

Wahusika wote wanatakiwa kuwa na sanduku (tranka), bima za afya kwa walionazo, aidha wanatakiwa wawe na fedha kiasi kwa matumizi binafsi na fedha nyingine kwa ajili ya kununulia vifaa vifuatavyo ambavyo hupatikana duka la Chuo:

  • Mashuka mawili (02) ya rangi ya bluu
  • Mto 01 na foronya 02 za rangi ya bluu
  • Chandarua 01 rangi ya bluu (duara)
  • Ndoo ya plastiki ya lita 20
  • Sahani na kikombe cha bati
  • Raba za michezo
  • Fulana
See also  Names Called for Census Job Interview | Majina ya Ajira za Sensa 2022 Munduli - Mjini Magharibi (Zanzibar)

SOMA MAELEZO KAMILI NA LIST YA MAJINA (PDF) HAPA – BOFYA HAPA

Spread the love

About Author

Here to ease your search for new opportunities. I am a person with a passion of sharing useful opportunities to interested Job seekers in a timely and accurate manner, aiming to ease the Job Search experience.