WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA KUJITOLEA MWAKA 2026.

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA KUJITOLEA MWAKA 2026.

WITO WA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA KUJITOLEA MWAKA 2026.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele, anawataarifu Vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani nafasi za kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2026.

Utaratibu wa Vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na Mafunzo hayo, unaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako mwombaji anaishi. Aidha, vijana wenye taaluma za:

  • Diploma in Information Technology
  • Diploma in Business Information Systems
  • Diploma in Computer Science
  • Diploma in Information and Communication Technology (ICT)
  • Diploma in Cyber Security and Digital Forensics
  • Bachelor of Science in Computer Science
  • Bachelor of Science in Information Technology
  • Bachelor of Science in Computer Engineering
  • Bachelor of Science in Business Information Technology
  • Bachelor of Science in Cyber Security and Digital Forensics
  • Bachelor of Science in Computer Networks and Information Security Engineering

na Vijana wenye Vipaji vya Michezo mbalimbali, wanashauriwa kujitokeza kwa wingi kupitia Mikoa yao.

Usaili wa Vijana hao kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea utaanza tarehe 26 Jan 2026 kwa Mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani. Vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye Makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia tarehe 27 Februari 2026 hadi 04 Machi 2026.

Aidha, Jeshi la Kujenga Taifa linapenda kuwataarifu Vijana watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi ajira, pia halihusiki kuwatafutia ajira katika Asasi, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyo ya Kiserikali, bali hutoa Mafunzo yatakayosaidia Vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza Mkataba wao na JKT.

See also  Call for Oral Interview at Dodoma City Council/ Wito wa Usaili wa Mahojiano - Majina 343

Sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo yanapatikana katika Tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.mil.tz

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, anawakaribisha Vijana wote watakaopata fursa hiyo kuja kujiunga na vijana wenzao ili kujengewa Uzalendo, Umoja wa kitaifa, Ukakamavu, Kufundishwa Stadi za Kazi, Stadi za Maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa lao.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano,

Makao Makuu ya JKT.


DOWNLOAD PDF BELOW:-

Spread the love

About Author

Here to ease your search for new opportunities. I am a person with a passion of sharing useful opportunities to interested Job seekers in a timely and accurate manner, aiming to ease the Job Search experience.