Various Job Opportunities At Ideon Limited September 2025

Full Time

Website Ideon Limited

Ideon Limited

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.

IDEON LIMITED inatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo kwa ajili ya kituo chake kilichopo Mbezi Beach, Dar es Salaam:

1. Msimamizi wa Wafanya Usafi (1 Nafasi)

Majukumu Makuu:

  • Kusimamia kazi za kila siku za wafanya usafi.
  • Kugawa majukumu na kuhakikisha maeneo yote yanasafishwa ipasavyo.
  • Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha viwango vya usafi vinafuatwa.
  • Kuwalindisha na kuwaongoza wafanya usafi kuhusu kanuni za usalama na afya.
  • Kuandaa taarifa fupi za kazi na maduhurio ya wafanyakazi.

Sifa na Uzoefu:

  • Awe na angalau Cheti au Diploma katika Utawala wa Biashara, Usimamizi wa Hoteli, au fani nyingine inayohusiana.
  • Uzoefu wa angalau mwaka 1-2 katika usimamizi au kazi za usafi.
  • Uwezo mzuri wa kuongoza na kuwasiliana.
  • Awe mwaminifu, mchapakazi na mwenye uwezo wa kufanya kazi bila kusimamiwa wa karibu.

Masharti ya Kazi:

  • Eneo la kazi: Dar es Salaam – Mbezi Beach
  • Mshahara: 180,000/= Tsh kwa mwezi (NET)

2. Wafanya Usafi (4 Nafasi)

Majukumu Makuu:

  • Kusafisha na kutunza usafi wa maeneo yaliyopangwa kila siku.
  • Kufanya kazi kwa kufuata ratiba na maagizo ya Msimamizi.
  • Kutunza vifaa na kuhakikisha vinatumika kwa uangalifu.
  • Kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni za usalama na afya.

Sifa na Uzoefu:

  • Awe na angalau elimu ya msingi/sekondari.
  • Awe na bidii, uaminifu na uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano.
  • Uzoefu wa kazi za usafi utapewa kipaumbele.

Masharti ya Kazi:

  • Eneo la kazi: Dar es Salaam – Mbezi Beach
  • Mshahara: 150,000/= Tsh kwa mwezi (NET)

Namna ya Kutuma Maombi:

  • Wasilisha CV yako kupitia barua pepe: info@ideon.co.tz

To apply for this job email your details to info@ideon.co.tz

Spread the love