Mfanyakazi wa Shamba (Mhudumu wa Mifugo) at Nyangureta Farm , Mwanza April 2026

Full Time
  • Full Time
  • Mwanza

Nyangureta Farm

Nyangureta Farm

NYANGURETA FARM – TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

Nafasi: Mfanyakazi wa Shamba (Mhudumu wa Mifugo) – Nafasi 1

Mahali: Mwanza

Aina ya Ajira: Ajira ya kudumu (Full-time)

Muhtasari wa Kazi:

Nyangureta Farm inatafuta mfanyakazi mwenye uzoefu na ujuzi katika ufugaji wa mifugo kujiunga na timu yetu ya shamba. Mwombaji atakayefanikiwa atakuwa na jukumu la kutunza mifugo kama ng’ombe na wanyama wengine wa shambani kwa kuhakikisha wanapata huduma bora na kuongeza uzalishaji.

Sifa na Ujuzi:

  • Angalau Stashahada (Diploma) au Shahada (Degree) katika Sayansi ya Ufugaji (Animal Science), Uzalishaji wa Mifugo, au fani inayohusiana.
  • Awe amesoma katika chuo kinachotambuliwa kinachotoa kozi hizo kama vile: SUA (Sokoine University of Agriculture), MATI (Mfano: MATI Tengeru, MATI Uyole), Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia au vyuo vingine vinavyotambulika.
  • Uzoefu wa kufanya kazi na mifugo, hasa ng’ombe, ni muhimu.
  • Uelewa wa afya ya mifugo, lishe na uzalishaji.
  • Uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea na kwa kushirikiana na timu.
  • Awe na afya njema na tayari kufanya kazi katika mazingira ya shamba.
  • Mwaminifu, makini na mwenye kujituma.

Majukumu ya Kazi:

  • Kutunza mifugo kila siku ikiwemo ng’ombe, mbuzi na wanyama wengine.
  • Kuhakikisha mifugo inapata chakula na maji ya kutosha kwa wakati.
  • Kufuatilia afya ya mifugo na kutoa taarifa mapema endapo kuna dalili za magonjwa.
  • Kushiriki katika shughuli za kukamua maziwa, uzalishaji na uangalizi wa mifugo.
  • Kudumisha usafi wa mabanda ya mifugo na mazingira ya shamba kwa ujumla.
  • Kusaidia katika utoaji wa chanjo na matibabu ya msingi chini ya uangalizi.
  • Kutunza kumbukumbu za uzalishaji, lishe na afya ya mifugo.
  • Kushiriki katika usimamizi wa malisho na uhifadhi wa chakula cha mifugo.

Jinsi ya Kutuma Maombi:

Waombaji watume maombi yao yakijumuisha CV na vyeti husika kupitia:
Barua pepe: mumangicstcoltd@gmail.com
Simu: 0755 107 588 / 0767 447 742
Mwisho wa kutuma maombi: 10 Mei 2026

To apply for this job email your details to mumangicstcoltd@gmail.com

Spread the love