Website Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC)
Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC)
Wahudumu wa Huduma kwa Wateja – Nafasi za Kujitolea (Customer Care Volunteers)
Kuhusu Tangazo (Overview)
Majukumu ya Kazi (Key Responsibilities)
-
Mapokezi na Mwongozo: Kuwapokea na kuwaelekeza wagonjwa na wageni kwa heshima, ukarimu, na weledi; kutoa taarifa sahihi kuhusu huduma, vitengo, na taratibu za hospitali; na kuwaelekeza kwenye maeneo au vitengo husika.
-
Kushughulikia Malalamiko na Maoni: Kupokea na kushughulikia malalamiko, maoni, na changamoto za wagonjwa na wageni; kufuatilia utatuzi wake kwa kushirikiana na vitengo husika; na kukusanya maoni ya wagonjwa kuhusu ubora wa huduma.
-
Usiri, Taarifa na Maboresho: Kuhakikisha usiri na faragha ya taarifa za wagonjwa wakati wote; kuorodhesha malalamiko, pongezi, na maoni ya wateja na kuwasilisha taarifa kwa viongozi husika; na kutambua changamoto za utoaji wa huduma na kupendekeza maboresho.
-
Mafunzo na Huduma Zinazomlenga Mgonjwa: Kushiriki katika mafunzo ya huduma kwa wateja na shughuli za kuboresha ubora wa huduma; kufuatilia utekelezaji wa maboresho yaliyopendekezwa; kuhamasisha utamaduni wa kumweka mgonjwa katikati ya huduma (patient-centred care); na kuandaa na kuwasilisha taarifa za huduma kwa wateja kwa msimamizi au kitengo husika.
Sifa za Mwombaji na Nyaraka Zinazohitajika (Qualifications & Required Documents)
-
Elimu: Awe amehitimu wa Kidato cha Nne (4) au Sita (6) mwenye Stashahada (Diploma) katika fani ya Maendeleo ya Jamii, Mawasiliano, Uhusiano, au sifa zingine zinazolingana na hizo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
-
Umri: Mwombaji awe na umri kati ya miaka 25 mpaka 30.
-
Viambatisho Muhimu: Mwombaji awasilishe barua ya maombi pamoja na nakala za vyeti vya Kidato cha Nne / Kidato cha Sita, vyeti vya taaluma, cheti cha kuzaliwa, pamoja na nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
Jinsi ya Kutuma Maombi (How to Apply)
To apply for this job email your details to kcmcadmin@kcmc.ac.tz
