Tangazo la Kuitwa Kwenye Usaili MDAs Na LGAs December 2025


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na.: JA.9/259/01/C/10
Tarehe: 03/12/2025


TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (kwa niaba ya MDAs & LGAs) anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 15/12/2025 hadi 22/12/2025.


MAELEKEZO MUHIMU KWA WASAILIWA

1. Tarehe, Muda na Mahali

  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe zilizooneshwa kwenye ratiba.
  • Muda na sehemu vimeainishwa kwa kila Kada.
  • Usaili utafanyika kulingana na mahali alipo msailiwa (Current Resident Region).
  • Vituo halisi vya usaili vitatolewa kupitia tovuti ya www.ajira.go.tz.

2. Vituo vya Usaili

  • Usaili utafanyika katika Mikoa yote ya Tanzania Bara pamoja na Vituo Maalum vya Unguja na Pemba.

3. Barakoa (Mask)

  • Kila msailiwa anatakiwa kufika eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa.

4. Kitambulisho (ID)

Kila msailiwa anatakiwa kuwa na kitambulisho halali kwa ajili ya utambuzi, ikiwemo:

  • Kitambulisho cha Mkazi
  • Kitambulisho cha Mpiga Kura
  • Kitambulisho cha Kazi
  • Kitambulisho cha Uraia
  • Hati ya Kusafiria
  • Leseni ya Udereva
  • Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji

5. Vyeti Halisi

  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI HALISI vyote, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kulingana na nafasi husika.

6. Nyaraka Zisizokubalika

Nyaraka zifuatazo hazitakubaliwa, na mwenye nazo hataruhusiwa kuendelea na usaili:

  • Testimonials
  • Provisional Results
  • Statement of Results
  • Matokeo ya Kidato cha IV & VI (Results Slips)

7. Usajili wa Bodi za Kitaaluma

  • Kwa kada zinazohitaji usajili, leta vyeti halisi vya usajili pamoja na leseni za kufanyia kazi.

8. Gharama

  • Kila msailiwa atajigharamia usafiri, chakula na malazi.
See also  TRA RATIBA YA USAILI WA VITENDO NA MAHOJIANO/ SCHEDULE FOR PRACTICAL AND ORAL INTERVIEWS 2025

9. Mavazi

  • Wasailiwa wanapaswa kuvaa mavazi nadhifu na yenye staha, kulingana na waraka wa mavazi.

10. Waliosoma Nje ya Tanzania

  • Vyeti viwe vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NACTVET, NECTA).
  • Kwa kada zinazohitaji GPA, leta cheti cha ukokotozi wa GPA kutoka TCU.

11. Namba ya Usaili

  • Wasailiwa wote wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao za Ajira Portal na kunakili namba ya usaili.

12. Majina Yanayotofautiana

  • Wasailiwa wenye tofauti za majina kwenye nyaraka wanapaswa kuwasilisha Hati ya Kiapo cha Kubadili Jina (Deed Poll) iliyosajiliwa na Wizara ya Ardhi.

RATIBA YA USAILI (MUHTASARI WA BAADHI YA KADA)

MWAJIRIKADATAREHE & MUDA
MDAS & LGASMWALIMU DARAJA LA III B โ€“ FIZIKIA2025-12-15 saa 07:00:00
MDAS & LGASMWALIMU DARAJA LA III C โ€“ KILIMO2025-12-16 saa 07:00:00
MDAS & LGASMSAIDIZI WA HESABU DARAJA LA II2025-12-16 saa 07:00:00
MDAS & LGASAFISA WA SHERIA DARAJA LA II2025-12-17 saa 07:00:00
MDAS & LGASMHANDISI KILIMO DARAJA LA II2025-12-17 saa 07:00:00
MDAS & LGASMSANIFU MAJENGO DARAJA LA II2025-12-17 saa 07:00:00
MDAS & LGASMWALIMU DARAJA LA III B โ€“ HISABATI2025-12-17 saa 07:00:00
MDAS & LGASAFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II2025-12-18 saa 07:00:00
MDAS & LGASMHASIBU DARAJA LA II (ACCOUNTANT)2025-12-18 saa 07:00:00
MDAS & LGASMWALIMU DARAJA LA III B โ€“ TEHAMA2025-12-18 saa 07:00:00
MDAS & LGASAFISA MIFUGO DARAJA LA II2025-12-19 saa 07:00:00
MDAS & LGASMWALIMU DARAJA LA III C โ€“ FIZIKIA2025-12-19 saa 07:00:00
MDAS & LGASMWALIMU DARAJA LA III B โ€“ BAIOLOJIA2025-12-22 saa 07:00:00

Kada zingine nyingi na orodha kamili ya majina ya wasailiwa yapo kwenye kurasa zinazofuata za tangazo husika.

Spread the love