Nafasi Ya Kazi: Mhudumu Wa Usafi Wa Hoteli (Housekeeping) – Shamool Hotel, Dar es Salaam November 2026

Full Time

Website Shamool Hotel

Shamool Hotel

NAFASI YA KAZI: MHUDUMU WA USAFI WA HOTELI (HOUSEKEEPING) – SHAMOOL HOTEL
Kampuni: Shamool Hotel
Mahali: Sinza, Dar es Salaam
Aina ya Ajira: Ajira ya Muda Wote (Full-Time)
Kuhusu Nafasi Hii:
Shamool Hotel iliyopo Sinza, Dar es Salaam inatafuta Mhudumu wa Usafi wa Hoteli (Housekeeping) mwenye uzoefu, anayejituma, mwaminifu na aliye makini katika kazi ili kujiunga na timu yetu.
Majukumu Makuu:
  • Kusafisha na kuandaa vyumba vya wageni kwa viwango vya juu vya ubora.

  • Kuhakikisha usafi wa vyumba, mabafu, na maeneo yote ya pamoja (public areas) muda wote.

  • Kusaidia kazi za dobi (laundry), ikiwemo kufua, kupiga pasi, na kupanga mashuka.

  • Kusaidia kutoa huduma kwa wageni na kushirikiana na idara nyingine pale inapohitajika.

  • Kufanya kazi kwa kujitegemea pamoja na kushirikiana vyema na wenzako.

Sifa za Mwombaji:
  • Awe na uzoefu wa kazi ya usafi wa hoteli (Housekeeping).

  • Uzoefu katika masuala ya dobi (laundry) na kusaidia idara nyingine utakuwa ni sifa ya ziada.

  • Awe na umakini, uaminifu, bidii, na nidhamu ya hali ya juu kazini.

  • Uwezo wa kujiongeza (kuona kazi inayohitajika na kuifanya bila kusubiri kuambiwa).

  • Moyo wa ushirikiano na utayari wa kujifunza kazi mbalimbali.

  • Kujua lugha ya Kiingereza ni faida ya ziada, lakini si lazima.

Jinsi ya Kutuma Maombi:
Waombaji wenye sifa wanatakiwa kutuma nyaraka na taarifa zifuatazo kwenda barua pepe info@shamal.com:
  1. Wasifu binafsi (CV).

  2. Maelezo ya uzoefu wako wa kazi.

  3. Kiwango cha mshahara unaotarajia kwa mwezi.

  4. Tarehe ambayo utakuwa tayari kuanza kazi.

Zingatia: Kichwa cha habari (Subject) kwenye barua pepe yako kiandikwe: Housekeeping – Shamool Hotel

To apply for this job email your details to info@shamool.com

Spread the love