Website Mascons Tanzania Limited
Mascons Tanzania Limited
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
JINA LA KAMPUNI: MASCONS TANZANIA LIMITED
MAHALI PA KAZI: Dar Es Salaam , Office : Ubungo Plaza, 2nd Floor
Mascons Tanzania Limited ni kampuni ya Kitanzania inayojishughulisha na shughuli za ujenzi, ukodishaji wa mitambo na mashine nzito, pamoja na usambazaji wa vifaa vya ujenzi. Kutokana na upanuzi wa shughuli zake, kampuni inakaribisha maombi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uzoefu kwa nafasi zifuatazo:
Nafasi Zinazohitajika
-
Backhoe Operators – Nafasi 5
-
Wheel Loader Operators – Nafasi 4
-
Self Loader Mixer Operators – Nafasi 4
-
Bulldozer Operators – Nafasi 2
-
Truck Tippers – Nafasi 6
Aina ya Ajira
Nafasi hizi ni za Casual Employment. Hata hivyo, utendaji mzuri wa kazi, nidhamu, uwajibikaji na kujituma vinaweza kumwezesha mwajiriwa kupewa ajira ya kudumu kulingana na mahitaji ya kampuni na tathmini ya utendaji wake.
Sifa za Waombaji
-
Awe na uzoefu wa kuendesha mashine au chombo husika.
-
Awe na leseni halali ya udereva inayoruhusu uendeshaji wa mashine au chombo husika.
-
Awe na uelewa wa taratibu za afya na usalama mahali pa kazi.
-
Awe na nidhamu, uaminifu, uwajibikaji na uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi.
Nyaraka za Kuambatanisha
-
Barua ya maombi.
-
Wasifu binafsi (CV).
-
Nakala za vyeti vya taaluma na mafunzo husika.
-
Nakala ya leseni halali ya udereva.
-
Majina na mawasiliano ya wadhamini wawili (Referees) wa karibu pamoja na utambulisho kutoka serikali ya mtaa.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Waombaji watume maombi yao pamoja na nyaraka zote zinazohitajika kupitia barua pepe:
mkumilafedrick@gmail.com
Mwisho wa kutuma maombi: Tarehe 31 Julai 2026.
Kumbuka: Ni waombaji watakaochaguliwa kwa hatua ya awali pekee ndio watakaoitwa kwenye usaili. MASCONS TANZANIA LIMITED inatoa fursa sawa za ajira kwa waombaji wote wenye sifa stahiki.
To apply for this job email your details to mkumilafedrick@gmail.com
