Website Fula General Services Company Limited
Fula General Services Company Limited
Nafasi za Kazi Fula General Services Company Limited, Dar es Salaam , June 2026 – Ajira Mbalimbali
FULA GENERAL SERVICES COMPANY LIMITED
P.O.BOX 45500 Temeke Dar Es Salaam | Phone: +255 754 037 344
Email: info@fulageneral.co.tz | Web: www.fulageneral.co.tz
Professionalism, integrity and Excellence
Tarehe: 14th June 2026
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Fula General Services Company Limited ya Dar es Salaam, anawatangazia Watanzania wote wenye bidii, nidhamu, uaminifu na utayari wa kufanya kazi, kuwa kampuni imefungua rasmi dirisha la kupokea maombi ya ajira.
Kampuni inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa vijana wa kike na wa kiume wachapakazi na wenye nidhamu ya hali ya juu kujaza nafasi zilizotajwa kwenye tangazo hili.
1. NAFASI ZINAZOSHINDANIWA NA MAJUKUMU YAKE
A. Afisa Masoko
Majukumu:
-
Kutafuta masoko mapya ya huduma za usafi na fumigation.
-
Kubuni na kusimamia mikakati ya kidijitali (social media) na ya ana kwa ana ya kujitangaza.
-
Kutengeneza mahusiano mazuri na wateja wa majumbani na maofisini.
-
Kuhakikisha malengo ya mauzo ya kampuni yanafanikiwa.
Sifa Maalum:
-
Awe mbunifu na mwenye ushawishi mkubwa.
-
Awe na uelewa wa masoko ya kidijitali.
-
Elimu ya Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) au Shahada (Degree) katika Masoko, Biashara au Uhusiano wa Umma itazingatiwa.
B. Wasaidizi wa Majumbani (Housemaids / Houseboys)
Majukumu:
-
Kufanya usafi wa nyumba.
-
Kufua nguo.
-
Kupika chakula.
-
Kusaidia majukumu ya kila siku ya nyumbani.
Sifa Maalum:
-
Awe mwaminifu, msafi na mwenye uwezo wa kufuata maelekezo.
-
Uwezo wa kusaidia watoto masomo ya nyumbani (Homework) utazingatiwa kama sifa za ziada.
C. Wafanyakazi wa Maofisini (Office Cleaners / Attendants)
Majukumu:
-
Kufanya usafi wa maofisi, korido na vyoo.
-
Kuhakikisha mazingira ya kazi yanabaki safi na nadhifu muda wote.
Sifa Maalum:
-
Awe na muonekano nadhifu.
-
Awe anayejituma.
-
Awe na lugha nzuri kwa wateja na wafanyakazi.
D. Mafundi, Usafi na Fumigation (Cleaning Fumigation & Technicians)
Majukumu:
-
Kufanya usafi wa kina (Deep Cleaning).
-
Kupiga dawa ya kuua wadudu (Fumigation) kwenye nyumba, maofisi na maeneo mbalimbali.
Sifa Maalum:
-
Awe tayari kujifunza matumizi ya vifaa vya kisasa vya usafi na kemikali.
-
Awe na nguvu na utayari wa kufanya kazi katika maeneo tofauti.
E. Wasimamizi wa Kazi
Majukumu:
-
Kusimamia uendeshaji wa kila siku wa shughuli za usafi na huduma za kampuni katika maeneo husika.
2. SIFA ZA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE
-
Uwe raia wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.
-
Uwe na tabia njema, nidhamu ya hali ya juu na usiri mkubwa wa kazi.
-
Kujua Kiingereza kwa nafasi za maofisini na masoko itakuwa sifa ya ziada.
-
Waombali wawe wahitimu wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne, au wenye elimu ya Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree).
3. MASLAHI KWA WAAJIRIWA
-
Mshahara mzuri na wa ushindani sokoni.
-
Mazingira salama, ya kuaminika na rasmi ya kiofisi ya kufanyia kazi.
-
Mafunzo ya mara kwa mara ya kuongeza ujuzi. Fursa ya kupanda ngazi kitaaluma kulingana na utendaji kazi.
4. MAOMBI YATUMWE KUPITIA ANUANI IFUATAYO
MTENDAJI MKUU (CEO)
FULA GENERAL SERVICES COMPANY LIMITED
S.L.P 45500
TEMEKE, DAR ES SALAAM
VIAMBATANISHO:
-
Nakala ya Kitambulisho cha NIDA au Kitambulisho cha kura.
-
Barua ya Utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa wako.
-
Picha mbili (2) za Passport Size zenye background ya bluu.
-
Vyeti vya elimu au taaluma husika.
-
Wadhamini wawili (2) wanaoaminika.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Maombi yatumwe kupitia moja kati ya njia zifuatazo:
-
WhatsApp: +255 754 037 344
-
Email: info@fulageneral.co.tz
MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI: Tarehe 31 Agosti 2026, saa 6:00 usiku.
WAHI SASA! NAFASI NI CHACHE NA USHINDANI NI MKUBWA.
Download Hapa – Tangazo_la_Ajira_Fula_General_Services – PDF Format
To apply for this job email your details to info@fulageneral.co.tz
