Nafasi 3 za kazi: Operations Manager – Lipa Airtel; Ihalula Company Limited, Sumbawanga, Rukwa Septemba 2026

Website Ihalula Company Limited

Ihalula Company Limited

Operations Manager – Lipa Airtel

IHALULA COMPANY LIMITED inakaribisha waombaji wenye sifa kuomba nafasi ya Operations Manager – Lipa Airtel (Nafasi 3).

Majukumu Makuu

  • Kusimamia shughuli zote za Lipa Airtel na kuhakikisha ufanisi wa operesheni.
  • Kutathmini mwenendo wa mauzo na kuandaa ripoti za kila siku, wiki na mwezi.
  • Kubuni na kutekeleza mikakati ya kuongeza wateja na miamala.
  • Kuhudumia wateja na kutatua changamoto zinazohusiana na huduma za Lipa Airtel.
  • Kushirikiana kwa karibu na Airtel katika utekelezaji na uboreshaji wa shughuli za Lipa Airtel.
  • Kusimamia na kuhamasisha timu kufikia malengo yaliyowekwa.

Sifa za Mwombaji

  • Awe na elimu ya Form Four na kuendelea.
  • Awe na uzoefu katika Sales au Operations.
  • Awe na uelewa wa Telecom na Airtel Money.
  • Awe na uwezo mzuri wa uongozi na usimamizi wa timu.
  • Awe na uwezo mzuri wa mawasiliano, ufuatiliaji na utatuzi wa changamoto.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Tuma maombi yako kupitia:

Email: recruitments@ihalulatraders.co.tz

Deadline

30 September 2026

Jiunge nasi katika kukuza na kuimarisha huduma za Lipa Airtel.

To apply for this job email your details to recruitments@ihalulatraders.co.tz

Spread the love