Website TTCL
TTCL
📢 FURSA YA KAZI
WAKALA WA USAJILI HUDUMA ZA FAIBA
TTCL Corporation
Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation linakaribisha vijana wenye uwezo uwezo wa ajili ya kazi ya Uwakala wa usajili wa wateja wa Faiba katika jiji la Dar es salaam.
1. SIFA ZA WAOMBAJI
-
Umri usiopungua miaka 18.
-
Awe raia wa Tanzania mwenye kitambulisho halali kimoja au zaidi kati ya vifuatavyo: Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Kitambulisho cha Mpiga Kura, leseni ya Udereva, au kitambulisho kingine kinachotambulika kisheria.
-
Awe na cheti cha kuhitimu Kidato cha Nne.
-
Awe anaishi Dar es salaam.
-
Awe na uwezo wa kusoma na kuandika Kiswahili na /au Kiingereza.
-
Awe na nidhamu, uadilifu, na asiwe na rekodi ya makosa yoyote ya jinai au mashtaka yanayohusiana na uaminifu.
-
Awe na uwezo wa kutumia simu janja (smartphone) kwa shughuli za kijidigitali.
-
Awe tayari kupokea mafunzo na kufuata taratibu za Shirika.
-
Awe na uwezo wa kujieleza na kuwasiliana na wateja.
2. TARATIBU ZA MAOMBI
-
Waombaji wote wafike TTCL Kijitonyama, wilaya ya Kinondoni, Dar es salaam tarehe 16/12/2025 kuanzia saa 03:00 asubuhi kwa ajili ya usaili wakiwa na viambatanishi elekezi.
Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia 0222 100 100 au barua pepe: dg@ttcl.co.tz
To apply for this job email your details to dg@ttcl.co.tz
