Website Mlimani Driving School
Mlimani Driving School
Wakufunzi Wa Udereva Wa Awali (Basic Driving Instructor) – Nafasi 10 & Wakufunzi Wa Udereva Wa Magari Ya Abiria Na Malori (PSV/HGV) – Nafasi 4 at Mlimani Driving School, Dar es Salaam na Bagamoyo September 2026
TANGAZO LA KAZI
Mlimani Driving School ni shule inayotoa mafunzo ya udereva wa magari madogo na ya abiria. Mlimani Driving School inahitaji wakufunzi wa udereva wenye WELEDI, UZOEFU na UADILIFU wa hali ya juu katika kazi.
1. WAKUFUNZI WA UDEREVA WA AWALI (BASIC DRIVING INSTRUCTOR) – NAFASI 10
-
Kituo cha Kazi: Dar es Salaam na Bagamoyo
Majukumu ya Kazi:
-
Kutoa mafunzo ya vitendo na nadharia kwa wanafunzi
-
Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya kwenda barabarani na wanafunzi ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo
-
Kutunza na kuandika daftari la safari za mafunzo (Logbook) kwa mafunzo ya kila siku ya vitendo (kuendesha gari)
-
Kutoa mafunzo ya udereva wa kujihami (Defensive Driving)
-
Kutoa muongozo kwa wanafunzi jinsi ya kujibu maswali na kujihami na matukio ya barabarani
-
Kuwatayarisha na kuwafundisha wanafunzi matukio ya dharura barabarani
-
Kuandaa masomo endelevu ya udereva na usalama barabarani ili kuwawezesha wanafunzi kufuzu mafunzo yao vizuri
-
Kuwapeleka wanafunzi kufanya majaribio ya udereva polisi baada ya kuhitimu mafunzo ili kuwezesha wanafunzi kupata leseni ya udereva baada ya kufaulu majaribio ya polisi (Traffic test)
-
Kufanya kazi nyingine atakayopagiwa na mkurugenzi au kiongozi wake
Sifa za Mwombaji:
-
Awe na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea
-
Awe na leseni ya Ukufunzi wa udereva iliyotolewa na jeshi la polisi
-
Awe na leseni ya udereva iliyo hai
-
Awe na cheti cha kidato cha nne (4) na mwenye ufaulu wa somo la Kiingereza na Kiswahili
-
Awe na uzoefu wa kufundisha udereva usiopungua miaka miwili (2) bila kusababisha ajali
2. WAKUFUNZI WA UDEREVA WA MAGARI YA ABIRIA NA MALORI (PSV/HGV) – NAFASI 4
-
Kituo cha Kazi: Dar es Salaam na Bagamoyo
Majukumu ya Kazi:
-
Kutoa mafunzo ya vitendo na nadharia kwa wanafunzi
-
Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya kwenda barabarani na wanafunzi ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo
-
Kutunza na kuandika daftari la safari za mafunzo (Logbook) kwa mafunzo ya kila siku ya vitendo (kuendesha gari)
-
Kutoa mafunzo ya udereva wa kujihami (Defensive Driving)
-
Kutoa muongozo kwa wanafunzi jinsi ya kujibu maswali na kujihami na matukio ya barabarani
-
Kuwatayarisha na kuwafundisha wanafunzi matukio ya dharura barabarani
-
Kuandaa masomo endelevu ya udereva na usalama barabarani ili kuwawezesha wanafunzi kufuzu mafunzo yao vizuri
-
Kuwapeleka wanafunzi kufanya majaribio ya udereva polisi baada ya kuhitimu mafunzo ili kuwezesha wanafunzi kuongeza madaraja ya leseni za udereva baada ya kufaulu majaribio ya polisi (Traffic test)
-
Kufanya kazi nyingine atakayopagiwa na mkurugenzi au kiongozi wake
Sifa za Mwombaji:
-
Awe na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea
-
Awe na leseni ya UKUFUNZI DARAJA B (Drivers Instructor Class B) iliyotolewa na jeshi la polisi
-
Awe na leseni ya udereva yenye daraja C na E iliyo hai
-
Awe hajasajiliwa na chuo chochote
-
Awe na cheti cha kidato cha nne (4) na mwenye ufaulu wa somo la Kiingereza na Kiswahili
-
Awe na uzoefu wa kufundisha udereva usiopungua miaka miwili (2) bila kusababisha ajali
MASHARTI YA JUMLA
-
Mwombaji awe raia wa Tanzania
-
Picha 3 za rangi za hivi karibuni (passport size)
-
Barua za wadhamini wawili zenye picha zao (passport) na anwani za makazi yao
-
Barua toka serikali ya mtaa unakoishi ikiwa na namba za simu za kiongozi wa serikali za mtaa aliyekupa barua hiyo
-
Waombaji wote waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV)
JINSI YA KUOMBA
Maombi yote yaambatanishwe na nakala za vyeti vya taaluma vilivyotajwa hapo juu na barua za maombi. Maombi yatumwe kupitia email: mlimanoverseas23@gmail.com au unaweza kuwasilisha maombi yako kwenye ofisi yetu yoyote itakayokuwa karibu kwako.
Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza.
Anuani ya Posta:
MKUU WA CHUO MLIMANI DRIVING SCHOOL S.L.P 34556 DAR ES SALAAM
-
Mwisho wa kupokea maombi: Tarehe 15/10/2026
To apply for this job email your details to mlimanoverseas23@gmail.com